Uamuzi wa mamlaka za Saudi Arabia kutekeleza mipango hiyo ulitangazwa wakati wa kikao na Mwanamfalme Saud bin Mishaal, Naibu Gavana wa Makka, kuhusu maandalizi ya msimu ujao wa Hija.
Maafisa wamesema kwamba mita za mraba 50,000 za njia zenye kivuli zinajengwa kwa waenda kwa miguu huko Mina, huku mita za mraba 60,000 za makao na feni za kutoa ukungu zikiwa zinawekwa karibu na Jabal al-Rahmah huko Arafat.
Hatua hii imechukuliwa huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu afya ya Mahujaji kutokana na hali ya joto kali na umati mkubwa.
Kikao kilitathmini maendeleo ya miradi inayoendelea ya kuwezesha ibada ya Hija mwaka huu kufanyika kwa njia ambayo itawaridhisha Mahujaji.
Mashirika yanayoshiriki yalitoa taarifa kuhusu utayari wa mipango yao ya kiutendaji na maendeleo ya miradi ya uboreshaji kwenye maeneo matakatifu.
Kamati pia ilichunguza mipango ya muda mrefu ya upandaji miti iliyolenga kupanda miti 10,000 ili kuboresha ubora wa hewa, kupunguza joto, na kuboresha hali ya Mahujaji.
Agenda nyingine kadhaa zilijadiliwa, na kamati ilitoa mapendekezo yanayohitajika.
342/
Your Comment